Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema ili kuinua viwango vya tafiti za vyuo nchini, vyuo vya elimu ya juu havinabudi kuendelea kuwekeza katika tafiti hususan za sayansi na teknolojia na kuhimiza ubunifu katika ufundishaji na ujifunzaji.
Makamu wa Rais amesema hayo aliposhiriki Mahafali ya 27 ya Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho mkoani Iringa. Ametoa wito kwa sekta binafsi kuunga mkono jitihada hizo kwa kuendelea kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu kwa kufadhili tafiti,kutoa ufadhili kwa wanafunziwa fani mbalimbali, kuanzisha vyuo vya elimu ya juu, kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu kwa kutoa nafasi za mafunz kwa vitendo na mafunzo kazini.
Aidha Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya elimu ya juu.Amesema uwekezaji katika mifumo ya TEHAMA utawezesha ufundishaji wa baadhi ya masomo kwa njia ya mtandao na hivyo kuongeza idadi ya wa tanzania watakaopata elimu ya juu.Ameongeza kwamba ufundishaji kwa njia ya mtandao utapunguza changamoto ya uhaba wa walimu ambapo mwalimu mmoja anaweza kuwafikia wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.
Hali kadhalika, Makamu wa Rais ametoa wito kwa VyuoVikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu nchini kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, ili kufundisha masomo na ujuzi muhimu unaokosekana nchini pamoja na ujuzi wenye wataalamu wa chache kama vile madaktari bobezi waupasuaji wa neva (neurosurgeon), upandikizaji wa uroto (none-marrowtransplant), upandikizajiwa figo (kidneytransplant), uhandisi wa roboti (roboticengineering), fizikia ya Nyuklia (nuclear physics), matumizi ya akilimnemba (application of artificial intelligence) na nano teknolojia (nano technology).
Vilevile amewasihi wahitimu kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini kama vile sekta za kilimo biashara, ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba, nishati jadidifu, matumizi ya teknolojia za kidijitali na TEHAMA, unenepeshaji wa mifugo, ufugaji wa nyuki, biashara na viwanda vidogovidogo ili kujipatia mitaji. Aidha, amewatahadharisha wahitimu kuhusu tabia ya kupenda mafanikio ya haraka pasipo kufanyakazi kwa bidii. Amewasihi kupenda kufanyakazi, kuepuka njia rahisi,kuwa waadilifu na waaminifu.
Makamu wa Rais amepongeza jitihada za Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu na atamizi ya Kiota(KiotaInnovationHub) ya Chuo Kikuu cha Iringa kwa kutoa mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali kwa wanafunzi na wajasiriamali.



Post a Comment