Mfanyabiashara na Msambazaji wa jezi za Simba SC Sandaland The Only One kupitia jopo la Wanasheria Wake amemtumia Demand Notice afisa habari wa Yanga Ally Kamwe kwa tuhuma za kumchafua.
Demand Notice hiyo inadai kuwa Ally alinukuliwa akisema Viongozi wa Simba wamemsusia bwana Sandaland uzinduzi wa jezi ndio maana amefanyia katika duka lake kwakuwa anawatia aibu jezi mbaya.
Mambo Matatu ambayo Sandaland anamtaka Ally Kamwe kufanya.
1) Kulipa fidia ya Bilioni 3
2) Kumuomba radhi binafsi hadharani
3) Kumuomba radhi katika vyombo vya habari kama anavyodai kumchafu ndani ya siku saba kutokea sasa.

Post a Comment