TUNATOA ELIMU KWA WANANCHI,SABABU TULIWAOMBA KUJIANDILISHA-ANNE MAKINDA

 


Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi mwaka 2022 Anne Makinda ametembelea Maonyesho ya48 ya saba saba yanayoendelea jijini Dar es salaam.


Akiwa katika viwanja hivyo vya Maonyesho Makinda ametembelea mabanda ya Bima,Banda la maridhiano,na Banda la Ofisi ya Takwimu (NBS).


Akiwa katika banda la NBS ameeleza waandishi wa habari kuwa Sensa ya mwaka 2022 ilikuwa na hatua tatu ambazo ni uhamasishaji wananchi waweze kujiandikisha, awamu ya pili ikawa ni ile siku ya kuhesabiwa na awamu ya Tatu ni kutoa elimu kwa wananchi wote .


"Tunatoa Elimu kwa wananchi kama mrejesho kwa sababu tuliwaomba kujiandikisha wakati huo tunawaambia faida ya Sensa"amesema.



Post a Comment

Previous Post Next Post