Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo katika mchakato wa mwisho wa kuweka stempu za kielektroniki (ETS) kwenye sukari na saruji ili kupunguza matukio ya ukwepaji kodi na kughushi.
Akizungumza katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) ambayo yanafanyika kila mwaka na kuandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Ndani wa TRA, Ndositwe Haonga alisema hatua hiyo itawasaidia walaji kununua bidhaa asilia bidhaa kutoka kwa wazalishaji.
Uanzishwaji unaotarajiwa wa stempu hizo za kidijitali kwa saruji na sukari ni baada ya kudanikiwa katika sigara, bia, mvinyo, vinywaji vikali na maji ya chupa ulioanza kutumika Januari 15, mwaka jana.
Haonga pia alisema hatua hiyo itakisaidia Mamlaka ya Mapato kukusanya ushuru zaidi utakaosaidia nchi kuboresha miradi ya maendeleo.
Alimalizia kwa kusema, "Ni furaha na heshima kubwa kuwakaribisha katika banda la TRA kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam ili kuelewa huduma zote tunazotoa."
Akizungumza awali, Ofisa Mwandamizi wa Usimamizi wa kodi kutoka TRA, Patric Massawe ametoa wito kwa watanzania kuitumia hakiki stempu kwa ajiri ya kupata bidhaa original na zenye ubora wa viwango.
Alisema kuwa watu wenye application za apple na android watakuwa na uwezo wa kukagua kujua kama bidhaa wanazonunua ni original na viwango kwa kulinda afya yao.
Hata hivyo, hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Mashimba Ndaki (Maswa Magharibi-CCM), alipendekeza stempu za kidijitali zitumike kwenye bidhaa nyinginezo kama vile saruji na sukari.
"Taratibu zinaendelea kwa kikao kati ya kamati na serikali kupitia TRA ili kupendekeza namna ya uwekaji stempu za kidijitali kwa bidhaa tajwa hapo juu na nyinginezo ili kuongeza ukusanyaji wa mapato," Bw. Ndaki alisema.
"Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa stempu za kielektroniki zimekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ushuru kwa serikali na hivyo zinapaswa kusambazwa kwa bidhaa nyingine ili kupunguza mianya ya ukwepaji kodi na kutangazwa kwa bidhaa zinazozalishwa."
Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi na kupendekeza kuwa umefika wakati sasa Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza muda wa matumizi ya kodi hiyo ya kielektroniki ili kupanua wigo wa kodi na kuongeza makusanyo ya mapato kwenye Hazina ya Taifa.
Mwisho

Post a Comment