Na Lucas Raphael,Tabora
Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuandikisha wapiga kura wapatao 259,988 mkoani Tabora kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 wa kuwapata Rais. Wabunge na Madiwani.
Mkurungezi wa Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi , Ramadhani Kailima alitoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza wadau kwa ajili ya maandlizi Uboreshaji wa Daftari kudumu la wapiga kura awamu ya Kwanza katika ukumbi wa mikutano wa Isike Mwanakinyungi mkoani Tabora..
Alisema idadi hiyo ya watu 259,989 ni sawa na ongezako la asilimia 17.8 ya Wapiga kura ya 1,4 waliopo kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura mkoani humo.
Aliendelea kusema kwamba Tume Baada ya kuandikishaji mkoa wa huo utakuwa na wapiga kura wapatao milioni 1.7.
Alisema kwamba idadi hiyo ya watu inaweza kuongezeka Kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kupiga kura wakati wa Uboreshaji wa Daftari la mwaka 2019/2020.
Kailima aliendelea kusema kwamba Tume ya Uchaguzi inatarajia kuwaondoa wapiga kura katika Daftari la kudumu la Uchaguzi wapatao 594,494 baada ya kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari Hilo..
Aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa kulingana na matokeao ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 wapiga kura wapya ni milioni 5.586,433 ambao wanatarajiwa kuandikishwa sawa na asilimia 18.7 Hadi kufikia mwaka 2025.
Alisema kwamba wapiga kura million 29,754,699 waliopo kwenye Daftari hilo baada ya Uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/2020, ambapo wapiga kura milioni 4,369,531 wanatarajia kuboreshewa Taarifa zao..
Hata hivyo mkurungezi huyo wa Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi alisema kwamba baada ya uboreshaj huo unatarajia wa Daftari litakuwa na Jumla ya wapiga kura Milioni 34,746,630 .
mwisho

Post a Comment