Jeshi la polisi limewafukuza kazi na kuwafuta jeshini askari Polisi wanne ,waliokuwa wanafanya kazi katika kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Mwanga, Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuwakuta na hatia ya kufuta picha kwenye camera za Jeshi la Polisi walizokuwa wanatumia kupima mwendo kasi (speed rader) wa madereva waliokuwa wamekiuka sheria za usalama barabarani, kwa maslahi yao binafsi.
Mei 30,2024, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kushikiliwa Askari Polisi wanne (4) kwa ajili ya uchunguzi na askari hao walishtakiwa kijeshi na walikuwa wanashikiliwa na Jeshi hilo kwa ajili ya uchunguzi.

Post a Comment