Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa ,amefanya mazungumzo na balozi wa Italia, hapa nchini,Marco Lombardi, ambaye amemaliza muda wake, Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu, amesema Tanzania, itaendelea kuwa mshirika muhimu na wa kimkakati wa nchi ya Italia.
Kwa upande wake Balozi Lombardi, amesema licha ya kumaliza muda wake kama balozi wa Italia nchini ,bado ataendelea kuisemea Tanzania na kuwa mhamasishaji wa fursa zilizopo.

Post a Comment