PUTIN ATUA KOREA KASKAZINI BAADA MIAKA 24 KUPITA

 Rais wa Urusi Vladimir Putin amefika Korea Kaskazini katika ziara inayoashiria kuimarika kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.



Putin amepokewa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika uwanja wa ndege wa Pyongyang, na kuelekea katika nyumba ya wageni ya Kumsusan ambako Putin atakaa.


Putin anafanya ziara yake ya kwanza Korea Kaskazini katika muda wa miaka 24, ameeleza katika taarifa iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari vya serikali saa chache kabla ya kuwasili kwake, kuwa anashukuru uungwaji mkono wa Korea Kaskazini kwa oparesheni maalum ya kijeshi ya Urusi ndani ya ardhi ya Ukraine.


Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini limeelezea mkutano kati ya Putin na Kim Jong Un kama tukio la kihistoria linaloonesha uimara wa urafiki wa dhati na umoja kati ya mataifa hayo mawili.



Post a Comment

Previous Post Next Post