Taarifa kutoka Ofisi ya Raisi nchini Malawi imesema kuwa ndege iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa nchi hiyo ,Saulos Chilima na watu wengine tisa imetoweka baada ya kuondoka katika Mji Mkuu Lilongwe leo Juni10,2024.
Rais Lazarus Chakwera amearifiwa kuhusu tukio hilo na kuamua kufuta ziara yake nchini Bahamas na kuamuru vyombo vyote nchini humo kuhusika katika kuitafuta ndege ilipo na kufanya uokoaji.
Tayari juhudi za kuitafuta ndege zimeanza lakini bado haijapatikana tangu kukatika kwa mawasiliano saa nne asubuhi za Malawi

Post a Comment