🔴🔴KENYA : RAIS RUTO ASITISHA KUSAINI MUSWADA

 KENYA: Rais William Ruto ametangaza kusitisha kusaini Muswada wa Sheria ya Fedha na kuagiza urejeshwe Bungeni kwaajili ya kufanyiwa maboresho kadhaa kabla ya Wabunge kwenda mapumziko. 



Aidha ikiwa Wabunge watafanyia kazi marekebisho hayo, Spika atalazimika kuurudisha kwa Rais lakini pia wanaweza kuupitisha tena bila Marekebisho ambapo upitishwaji wake utapaswa kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge nchini humo


Rais Ruto anahutubia Taifa muda huu ikiwa ni Hotuba ya pili baada ya nyingine aliyoitoa Juni 25, 2024 wakati kukiwa na Maandamano ya Vijana wanaopinga Muswada huo kupitishwa na Bunge


Post a Comment

Previous Post Next Post