HATIMAE TRY AGAIN AJIUZULU SIMBA



 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Salim Abdallah Muhene (Try Again) ametangaza rasmi kung’atuka katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC uamuzi ambao unaashiria MO Dewji anarudi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.


“Sisi kama Viongozi imefikia hatua sasa tuiokoe Simba SC, mtu pekee ambaye naona anaweza kuitoa hapa Simba na kuipeleka mbele zaidi ni MO Dewji, sijui kama ataridhia ila nimemuomba MO Dewji arudi kuwa Mwenyekiti wa Bodi” Salim Abdallah


Try Again alianza kushika nafasi ya juu ya Uongozi ndani ya Simba SC 2017 kama Kaimu Rais wa Simba SC, Mjumbe wa Bodi na hatimae Mwenyekiti wa Bodi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post