BANK YA TAIFA YA BIASHARA (NBC) KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WATEJA MKOANI DODOMA

 

Na VALENTINE OFORO

Benki ya Taifa ya Biashara kupitia timu ya kitengo cha Biashara na Uwekezaji (CIB), imefanya Ziara ya kukuza ushirikiano  pamoja na ubunifu kwa wateja katika tasnia ya Benki Mkoani Dodoma.


 


Aidha katika ziara hii, Timu ya NBC ilipata nafasi ya kumsalimu Mhasibu Mkuu wa Serikali Ndg. Leonard Mkude katika Ofisi za Wizara ya Fedha Jijini Dodoma pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA, Eng.Victor Seff katika Ofisi za TARURA zilizoko Mtumba Dodoma


 



Ushirikiano baina  ya taasisi za kifedha na wateja ni muhimu kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya mazingira ya ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia. Hivyo benki ya NBC imefanya ziara hii kama sehemu ya  kuwasikiliza wateja  na kuboresha huduma  ili kukidhi mahitaji yao.


 



Akizungumza wakati wa hafla  ya chakula cha jioni, iliyoandaliwa na NBC katika viwanja vya Collina Hoteli ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya wateja. Mkurugenzi wa wateja wakubwa NBC, Bw.James Meitaron, Amesema “Tunaamini kuwa ufunguo wa kuwa mtoa  huduma wa kipekee ni kuelewa mahitaji na matakwa ya wateja wetu. Hivyo kupitia ziara hizi tunapata mapendekezo na ushauri wenye suluhu zenye ubunifu wa kuboresha uzoefu wa kibenki kwa ujumla”


 


Wateja waliohudhuria hafla hii, wameonyesha kufurahishwa na mkakati huu wa NBC connect wenye lengo la kugusa biashara zao. Ambapo wamepata fursa ya kueleza changamoto zinazowakumba na kutoa ushauri ambao utarahisisha zaidi shughuli na huduma za kifedha mkoani humo.


 


Benki ya taifa ya biashara NBC wameahidi kuendelea kujali na kusikiliza matakwa ya wateja wao ambapo hivi karibuni wanatarajia kuendeleza ziara hiyo katika mkoa wa kanda ya ziwa ambao ni Mwanza pamoja na mkoa uliopo kanda ya kaskazini Arusha.

Post a Comment

Previous Post Next Post