Real Madrid wanafuzu kucheza fainali yao ya 15 ya UEFA Champions LEague kwa kuitoa FC Bayern Munich kwa ushindi wa 2-1 (agg 4-3), Bayern ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 68 kupitia kwa Alphonso Davies.
Real Madrid ambao kabla ya mchezo wa leo walikuwa hawajafungwa kwa mechi 20 mfululizo waliendelea kuwa watulivu hadi Joselu alipofunga magoli mawili ya ushindi kwa Real Madrid dakika ya 88 na 90+1.
Ushindi huo sasa umeifanya Real Madrid kufuzu kucheza fainali ya Champions League kwa mara ya 15 wakiwa wamewahi kutwaa mara 13 na sasa watacheza fainali dhidi ya Borussia Dortmund Juni 1 2024 katika uwanja wa Wembley uliyopo katika jiji la London Uingereza.
Wembley stadium 🏟️ ndiko Mchezo wa Fainali UEFA champions league utakako chezwa Tarhe 1/6.
Ni Borrussia Dortmund Vs Real Madrid.


Post a Comment