🔴🔴MAAFA AFRIKA KUSINI JENGO LAPOROMOKA LAUA

 


HABARI: Watu wanne wamefariki dunia na wengine 24 wameokolewa huku 51 wakiwa chini ya vifusi, baada ya jengo kuporomoka katika mji wa George Afrika Kusini.


Mamlaka katika eneo hilo imesema wafanyakazi 75 wa ujenzi walikuwa kwenye eneo la tukio wakati jengo la ghorofa tano likiporomoka huku sababu ya kuanguka kwa jengo hilo bado haijajulikana.


Taarifa za muda huu zinadai kuwa waokoaji wamekuwa na mawasiliano na baadhi ya watu chini ya vifusi.

Post a Comment

Previous Post Next Post