Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imedhamiria kuendelea Kutoa huduma za kimashtaka karibu na wananchi kadri wanavyoendelea kupata Fedha ili kuleta tija na ufanisi katika Utendaji wa kazi.
Akifungua mkutano maalum wa baraza la wafanyakazi ofisi ya Taifa ya Mashtaka Leo jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Baraza Hilo Bi. Javelin Rugaihuruza amesema Bajeti ya mwaka 2024/2025 itasaidia kuondoka changamoto Mbalimbali ikiwemo upungu wa watumishi na magari.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tawi la TUGHE NPS Bashiru Njoki amesema wajibu wa mtumishi ni kuzingatia nidhamu na Taratibu za kiutumishi katika Kutoa huduma kwa wananchi.
Baraza la wafanyakazi ofisi ya Taifa ya Mashtaka wamekiti leo kwa lengo la kujadili Mapendekezo ya Bajeti ya mshahara Kwa mwaka 2024/2025 pamoja na Mapendekezo ya mpango na Bajeti Kwa mwaka 2024/2025.


Post a Comment