VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KUTOA ELIMU KWA WATOTO

 MKUU wa Wilaya ya Chamwino Janeth Mayanja  amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuimarisha elimu ya kiroho inayotolewa kwenye nyumba za ibada,kwa ajili ya watoto ili taifa liweze kuwapata viongozi waliokamilifu na wenye hofu wa mbele za Mungu



Mayanja  ambaye alimwakilisha Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyemule alisema hayo alipokuwa akizungumza kwenye ibada ya Jumatatu ya Pasaka iliyokuwa imeandaliwa na Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Dodoma iliyofanyika Dodoma

 

Akizungumza na viongozi wa dini waliojumuika na waumini wao kutoka makanisa mbalimbali,alisema kuwa watoto hao wakiandaliwa kwa kupatiwa elimu ya kiroho wangali wadogo,Taifa litakuwa linawapata  walio kamilifu kiroho mbele za Mungu na hata kwa watanzania wenyewe.


Alisema kuwa kwa upande wa serikali inategemea sana madhehebu ya dini kwa kupitia viongozi wake katika kuwaelea watoto kiroho na kimwili,hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha mnashiriki kikamilifu kuwapatia elimu hiyo ambayo itawawezesha kushika nafasi mbalimbali za uongozi.


"Serikali inawategemea sana nyinyi viongozi wa madhehebu ya dini kutokana na mchango wenu wa kuwaandaa watoto ili waweze kuwa viongozi wa ngazi mbalimbali ziwe za kiserikali,kidini mashika taasisi au ndani ya familia,hivyo imarisheni mafundisho kwenye nyumba zenu za ibada mnazozitoa kwa watoto hao"alisema 



Aidha aliwaomba viongozi hao wa madhehebu ya dini kuendelea kuikumbuka serikali kwa kuimbea ili kudumisha amani na ifanikishe kutimiza malengo ya kukamilisha miradi yotekwa wakati ikiwemo ya kiafya,kilimo,umeme,barabara na elimu.


Awali wakisoma risala yao ya Umoja huo wa Madhehebu ya Kikristo Dodoma kwa Mkuu huyo wa wilaya Mwenyekiti wa Umoja huo Askofu Anthony Mlyashimba ameiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la pili watendaji wa idara ya ardhi kutokana na watumishi wake kufanya kinyume na viapo vyao.kanuni na sheria 


Askofu huyo alisema kuwa pamoja na jitihada zako nyingi unazozifanya za kuhakikisha watendaji hao wanafanya kazi kama walivyoahidi kwenye viapo vyao,bado migogoro ya ardhi inaendelea kuwepo kutokana na utendaji wanaoufanya kwa wananchi.


Hata hivyo Umoja huo wa madhehebu ya kikristo wameiomba serikali kutunga sheria kali za kudhibiti vitendo vinavyovunja heshima na utu wa mwanadamu,ili kurudisha jamii kwenye maadili mema na Taifa kuwa na watu wenye kumcha Mungu na kujiepusha na uovu.

MWISHO.

Post a Comment

Previous Post Next Post