Jeshi la polisi Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Jeshi la uhamiaji limekamata Watu 16 Raia wa Ethiopia wakisafirishwa kwa kutumia gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 katika eneo la Msitu wa Lunganga kata ya Sao Hill Tarafa ya Ifwagi Halmashauri ya mji wa Mafinga Wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Iringa, kamishna Msaidizi Mwandamizi Allan Bukumbi amethibitisha kuwa Wahamiaji hao wasio na vibali walitekelezwa katika mashamba ya Mahindi baada ya kushushwa kwenye gari ambalo awali lilisomeka kwa namba bandia za STL 3999 ambapo Dereva wa gari hilo alitekeleza gari hilo na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda Bukumbi amesema uchunguzi wa awali umeonesha kuwa gari hilo lilikuwa limesajiliwa kwa namba T 803 CVW likimilikiwa na Said Hassan mkazi wa Tabata Dar es salaam.
Hili linakua gari la tatu aina ya Land Cruiser V8 kukamatwa likiwa na Wahamiaji wasio na vibali ambapo mengine mawili yalikamatwa ndani ya siku 15 zilizopita Mkoani Manyara.

Post a Comment