Kikosi cha Timu ya Tabora United kesho kitashuka katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi , kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania bara, dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa saa 16:00jioni.
Tabora united chini ya kocha Mkuu Denis Goavec, mapema leo imekamilisha mandalizi yake kuelekea kwenye mchezo huo, na kwamba wachezaji wote wapo vizuri, hivyo kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kuzisaka alama tatu muhimu.
Nyuki hao wa Tabora, wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kugawana alama katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, uliopigwa kwenye uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera, na kwamba wachezaji, pamoja na benchi la ufundi, wamejidhatiti kuwapa furaha mashabiki wa Tabora.
Kwa upande wa Afya za wachezaji, kila mmoja yupo vizuri na kwamba wachezaji wote wanahari ,na morali ya kuhakikisha kuwa, wanakwenda kufanya vizuri kwenye mchezo huo ,licha ya kuwa Kagera imekuwa na ubora, lakini pia hata kwenye msimamo wapo kwenye nafasi nzuri.
“Tunakwenda kwenye mchezo wetu wa kesho, tukifahamu kabisa tunakutana na Timu nzuri, yenye wachezaji na benchi la ufundi lenye ubora, tumeifuatilia Kagera Sugar wamekuwa na matokeo mazuri, lakini hata kwenye msimamo pia wapo vizuri, ila kama Nyuki wa Tabora tutakwenda kupambana.
Katika mchezo uliopita tulipata matokeo ya sare dhidi ya JKT Tanzania, licha ya kwamba tulikuwa na mchezo mzuri, lakini tunasema sikuzote Timu bora haisare mara mbili, kesho tunakwenda kupambania alama tatu muhimu, kwa ajili ya masilahi mapana ya mkoa wetu wa Tabora na mashabiki kwa ujumla.
Tabora United inakwenda kwenye mchezo wa kesho ikiwa na jumla ya alama 22 ,huku ikiwa imecheza michezo 22 na hivyo kuendelea kusalia kwenye nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara.
Mwisho.

Post a Comment