Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inaendelea na zoezi la ukaguzi wa matumizi ya mionzi nchini kwa lengo la kujiridhisha kama matumizi ni salama katika maeneo ya hospitalini, viwandani, vituo vya utafiti, migodini, bandarini, viwanja vya ndege pamoja na katika ujenzi wa barabara na reli.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania TAEC Dkt. JUSTIN NGAILE baada ya kufanya ukaguzi katika hospitali ya wilaya ya Chato na Hospitali ya Rufaa ya Chato ambapo amesisitiza matumizi ya mionzi nchini ni lazima ya simamiwe vizuri ili kuwalinda wananchi, wafanyakazi na mazingira.
Katika Ukaguzi uliofanyika Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga Mkaguzi Mwandamizi wa Mionzi wa TAEC LAZARO MEZA akiwa mkoani Tanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bombo amesema zoezi la ukaguzi linaendana sambamba na kuwahamasisha wadau kutumia mifumo ya Tehama katika uombaji wa vibali vya umiliki wa vyanzo vya mionzi.
Kwa upande wake Msimamizi wa wafanyakazi wanaofanya kazi katika mashine za mionzi Hospitalai ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ya ATHUMAN MTOPA ameipongeza TAEC kwa mafunzo wanayotoa kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika vyanzo vya mionzi kwani yanawaimarisha katika utendaji wao wa kazi.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania PETER NGAMILO amesema TAEC inaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu faida na madhara ya mionzi.


Post a Comment