SERIKALI YAWAJENGEA UWEZO MAAFISA UNUNUZI NA UGAVI KUHUSUANA OZONI

 Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi.Kemilembe Mutasa ameeleza kuwa katika kutekeleza shughuli za Itifaki Serikali imeandaa na inatekeleza Mpango wa kuondosha Kemikali zinazomong'onyoa Tabaka la Ozoni jamii ya Hydrochlofluorocabons (HCFCs) ifikapo mwaka 2030.



Bi.Mutasa ameeleza hayo leo Machi 8,2024 jijini Dodoma wakati akifungua warsha ya Mafunzo kwa maafisa ununuzi na Ugavi kuhusu utekelezaji wa Itifaki ya Montreal inahusu Kemikali zinazomong'onyoa Tabaka la Ozoni



Ameeleza kuwa chini ya Mipango hii mojawapo ya Shughuli zinazotekelezwa na zinazopaswa kutekelezwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa maafisa ununuzi na Ugavi kutoka katika taasisi mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Itifaki husika ikiwemo utekelezaji wa kanuni za usimamizi wa Mazingira,udhibiti wa Kemikali zinazomong'onyoa Tabaka la Ozoni za Mwaka 2022


"Serikali inawataka maafisa ununuzi na Ugavi kuzingatia ukomo wa matumizi ya Kemikali na vifaa vyenye Kemikali zinazodhibitiwa chini ya Itifaki hii ikizingatia kwamba ndio wahusika wakuu katika kushughulikia ununuzi wa vifaa mbalimbali katika maeneo ya Kazi," Ameeleza


Aidha ameeleza kuwa Serikali iko katika maandalizi ya Mpango wa utekelezaji wa Marekebisho ya Kigali ya kupunguza matumizi ya Kemikali jamii ya hidrofluorokaboni.


"Naamini leo mtajenga uelewa mkubwa zaidi katika masuala ya Tabaka la Ozoni na hatimaye kuwa mabalozi wa kueneza elimu ya Ozoni kwa wengine ili sote kwa pamoja tuongeze juhudi za kuhifadhi Tabaka la Ozoni na hivyo kuokoa maisha duniani"Ameeleza



Katika hatua nyingine ameeleza kuwa Wanasayansi walivumbua kwamba baadhi ya Kemikali zinazotengenezwa na binadamu hujipenyeza angani na kumong'onyoa Tabaka la hewa ya Ozoni.


Pia Kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni ni Kemikali gesi zinazotumika katika majokofu na viyoyozi mbalimbali 



Hata hivyo ameeleza kuwa matokeo ya uvumbuzi huu yalisababisha Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mazingira (UN ENVIRONMENT) kufanya tathimini ya kisayansi na kuamua kuchukua hatua madhubuti kulinda tabaka la Ozoni.


Itifaki ya Montreal imekuwa ikifanyiwa marekebisho mbalimbali kutokana na tafiti zinazoainisha Kemikali ambazo zinazomong'onyoa Tabaka la Ozoni au kuwa na athari nyingine za kimazingira kama kusababisha ongezeko la joto duniani.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika warsha hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Catherine Bamwenzaki amesema kuwa Tanzania ni nchi Mwanachama wa Itifaki ya Montreal inayohusu udhibiti wa Kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni


"Madhumuni ya Itifaki ni kulinda afya ya binadamu na Mazingira dhidi ya madhara yanayotokana na kumong'onyoka kwa tabaka la Ozoni"Amesema 



Aidha ameongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imekuwa ikishirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania,Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Shirika la Viwango Tanzania na vyuo mbalimbali vya mafunzo ya ufundi katika kutoa mafunzo kwa maafisa mbalimbali kuhusu usimamizi na udhibiti wa Kemikali na vifaa vyenye Kemikali.




Post a Comment

Previous Post Next Post