Hii ni baada ya kutokea vuta ni kuvute kati ya mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Prince Dube na klabu yake ya Azam FC,
Sasa klabu ya Al Hilal ya Sudan inayofundishwa na kocha Florent Ibengé imegonga hodi katika klabu ya Azam FC na kutoa ofa ya Dola 200,000 (Tsh Milioni 509) ili kumnasa mshambuliaji huyo,
Hata hivyo ofa hiyo imekataliwa na Azam FC ambao wamesema dau la kumchukua mchezaji huyo ni Dola 300,000 (Tsh Milioni 764) kama mkataba wake unavyosema
Mkataba wa Prince Dube na Azam Fc amebakisha mkataba wa miaka miwili na nusu Azam FC utakaomuweka kwenye timu hiyo mpaka mwaka 2026.
Taarifa kutoka ndani ya Chanzo chetu cha kuamini kutokea Upande wa Prince Dube kimethibitisha kuwa Prince Dube kwasasa hafikirii kurejea Azam Fc na hata kujiunga na klab nyingine yoyote ILA tu Lengo kuu kuachana na klab hiyo na kuwa mchezaji huru.

Post a Comment