Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia SuluhuHassan amesema katika jukumu alilonalo la kuibeba Ajenda ya Nishati safi ya kupikia barani Afrika itawezesha kuhifadhi misitu na kulinda mazingira nchini.
Mhe. Rais amesema hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na washiriki wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Amewahimiza wanawake nchiniTanzaniakutekelezayatakayozungumzwa katika kongamano hilo na kuwaahidi serikali itaunga mkono yale yatakayotekelezwa katika
matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Akifungua Kongamano hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema wakati Serikali inakamilisha taratibu za kuanzisha mfuko wa nishati safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu bei ya gesi, ni vema
wadau mbalimbali kusaidia utekelezaji kupitia mikopo midogomidogo, vikoba
au vikundi vya wanawake ili kuhakikisha wanwake wanapata vifaa vya nishati
safi.
Aidha ameitaka Wizara ya Fedha kutazama uwezekano wa kupitia viwango vya kodi kwa majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia ili wananchi waweze kumudu kununua majiko hayo kwa urahisi.
Makamu wa Rais amehimiza vijiji na watu binafsi wanaopata mapato kutokana na biashara ya kaboni kutumia mapato hayo kugharamia nishati safi ya kupikia.
Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa taasisi za utafiti, sekta binafsi na wadau wengine kubuni teknolojia rahisi na zitakazopatikana kwa gharama nafuu ili kuharakisha uhamaji kutoka kwenye matumizi ya nishati chafu.
Amesema teknolojia zinazohitajika ni pamoja na zile za kupata majiko
yanayotumia nishati safi kuwezesha kupika chakula kinachoiva kwa muda
mrefu kama maharage na kande badala ya kutumia mkaa au kuni.
Pia ametoa wito kwa sekta binafsi kuunga mkono na kuchangia katika
kampeni ya kuondokana na matumizi ya nishati chafu. Amesema ni muhimu
Sekta binafsi kutumia mifuko ya Wajibu kwa Jamii kuwezesha kaya na taasisi
zinazowazunguka kupata nishati safi ya kupikia mjini na vijijini.
Makamu wa Rais ametoa wito wadau wote kuandaa programu mbalimbali
zitakazotoa elimu na hamasa kwa jamii nchi nzima ili kuongeza uelewa juu ya
matumizi ya nishati safi ya kupikia. Ameviasa vyombo vya habari na Asasi za
kiraia kuibeba ajenda ya nishati safi ya kupikia na kuwa mstari wa mbele
katika kuielezea kwa umma wa Watanzania. Amesema Vyombo vya habari
vinao wajibu muhimu wa kuelezea umma kuhusu madhara ya kuendelea
kutumia nishati chafu ikiwemo kupoteza misitu, mmomonyoko wa udongo,
kuongeza gesijoto, magonjwa ya mfumo wa hewa na madhara ya kiuchumi
kama watoto wa kike kushindwa kumaliza masomo.
Makamu wa Rais amesema Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan imetoa kipaumbele cha juu kukuza matumizi ya nishati safi ya
kupikia hapa nchini kwenye ajenda ya Taifa ya maendeleo pamoja na kuongeza rasilimali kuhakikisha ajenda hiyo inafanikiwa. Amesema Rais
amefanya maamuzi makubwa ikiwemo kuunda Kamati ya Kitaifa itakayosimamia utekelezaji wa ajenda hiyo, kuanzisha mfuko wa nishati safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini
kumudu bei ya gesi na kuchagiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa taasisi za Serikali zinazohudumia watu zaidi ya 100 kwa siku.





Post a Comment