KONGAMANO LA WANAWAKE LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA JAMII YATAKIWA KUBADILIKA

 


Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isidori Mpango ameshiriki Kongamano la wanawake kuhusu nishati safi ya kupikia Kongamano lililoandaliwa na wizara ya Nishati likifanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko katika ukumbi wa mikutano wa JAKAYA KIKWETE



Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati,  Mhe. Biteko amesema katika kuleta mabadiliko ya Matumizi ya Nishati Safi na Salama mwanamke mwenyewe anatakiwa kuwa mstari wa mbele


" kwenye ajenda hii batani ya kuleta mabadiliko ya nishati safi ya kupikia hapa Nchini ni mwanamke mwenyewe wa Tanzania",


 "Huyu akiweza kuibeba ajenda akaichukua kama ajenda yake watu wengine watafuata",


"Mungu amempa uwezo wa pekee, uwezo wa kibaiolojia lakini na upana wa ubongo wao,  amemuumba kwa namna ya ajabu sana ,tena ya kupendeza",


"Amempa tumbo si tu linatumika kwenye mmeng'enyo wa chakula bali limebeba uhai wa binadamu ndani yake,  Mungu amempa uwezo mwanamke wakufanya Jambo zaidi ya moja 


kwa wakati mmoja tofauti sana na mwanaume "


"Mungu amempa uwezo mwanamke wa kusema kidogo na kutenda zaidi ,Mungu amempa uwezo mwanamke wakuwa sababu ya furaha kwa viumbe wengine Duniani


"Kwakweli kama unamwanamke aliyewezeshwa anayejali nishati safi ya kupikia 





hutatumia muda mwingi kuzungumzia nishati safi ya kupikia the bali mwanamke ataisukuma ajenda hii" amesema Dkt. Dotto Biteko.

Kwa upande wa TFS

Akizungumza na vyombo vya habari Mhifadhi Anna Lyauo katika banda lao amesema Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ni mdau mkubwa katika kuhakikisha kwamba matumizi safi ya Nishati



"Ile Nishati chafu ni ile inayotokana na matumizi ya kuni,kuni zenyewe ukizichoma zinatoa hewa ya kaboni ambayo inaenda kuchafua anga"amesema


"Sisi tunahamasisha watu wasikate miti ili tuwe na hali ya hewa nzuri,hivyo watu watumie gesi ambayo ndiyo Nishati Safi kwa sababu yenyewe ukiitumia haina madhara katika anga"amesema



Aidha amesema TFS wameendelea kuhamasisha watu wapande miti ni katika kuokoa hali ya anga ambayo tayari ishachafuka na kuongeza kuwa viongozi mbalimbali wa Serikali wanaungana katika kuhakikisha miti haikatwi



Kuhusu kutoa elimu kwa jamii juu ya Utunzaji wa Mazingira amesema kuwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS ina vipindi mbalimbali ambavyo ni vya kuhamasisha watu kutokutumia kuni,ikiwa ni pamoja na kutumia maonyesho mbalimbali, vipindi vya radio, vipindi vya TV ambavyo vinatangaza na kuhamasisha Umma watumie gesi badala ya kuni ili kuweza kuhifadhi zaidi Mazingira


"Lakini pamoja na hayo tuna gari ambalo lina sinema linatembea katika maeneo mbalimbali hususani katika zile sehemu ambazo hazina umeme na hazifikiki kwa urahisi lengo ni kuhamasisha watu wasikate miti"




(Imeandikwa na Manase Madelemu)

Post a Comment

Previous Post Next Post