NI WAKATI WA UTALII KUSINI MWA TANZANIA

 

Na Richard Mrusha  Katavi 


Imeelezwa kuwa Hifadhi zilizopo kusini mwa Tanzania zinavivutio vingi lakini hazina umaarufu kama zingine 



Afisa Uhifadhi  daraja la pili Beatrice Msuya 

Amesema hifadhi ya Taifa Katavi pamoja na kutokusikika masikioni mwa wengi imesheeni vivutioa lukuki .


Hayo ameyasema Februari 28,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliotembelea hifadhi hiyo 



Amesema vivutio hivyo kuwa ni makundi makubwa ya Simba, Tambo, Nyati, na wanyama wengine, mbali  na wanyama hao kuna ziwa zuri na la kipekee ambalo limesheheni viboko Mamba na samaki aina ya Kambare, kamongo.


" hifadhi yetu inasifa ya kuwa na viboko wengi kuliko hifadhi zingine hapa nchini, kwa wingi huo inaiweka kuwa hifadhi  namba moja  kwa  viboko wengi."


Amesema Msuya kupitia ziwa hilo kuna utalii wa uvuvi wa samaki (spot fishing)

 Ambao unakuwa ni sehemu ya kuwachangamsha watalii wanaotembelea hifadhi hiyo na wamekua wakifanya hivyo kwa kushindana kupata samaki mwenye uzito mkubwa kuzidi wengine 


Ameongeza kuwa utalii huo wa uvuvi umekuwa chachu kwa hifadhi hiyo ambapo samaki waliovuliwa na kupimwa kisha uachiliwa na kurudi ziwani.


Amesema shughuli za uhifadhi ndani ya hifadhi hiyo zinahusisha kutambua mila na tamaduni za eneo hilo la katavi.

,"ifakapo jurai wakazi wa katavi huja hapa kufanya mambo yao ya mila na sisi tunawapa vibali vya kuingia ndani ya hifadhi kitendo hiki kimekuwa kivutio kwa baadhi ya watalii pia kina tusaidia kutunza mazingira 


Pia amewaamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kutalii haswa kwenye hifadhi ya Taifa Katavi kwasababu ina upekee wa aina yake.



Post a Comment

Previous Post Next Post