NDEGE YA TIMU YA AL-AHLY YAPATA ITILAFU GHANA




 Uongozi wa Al Ahly ya Misri wameiomba CAF isogeze mbele mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana baada ya ndege yao waliyokuwa wanasafiria kupata hitilafu katika jiji la Accra Ghana na kushindwa kuunganisha moja kwa moja katika mji wa Kumasi Ghana ambako utachezwa mchezo huo.


Mchezo ulikuwa uchezwe kesho Ijumaa ila wameomba uchezwe Jumamosi ili kuwapa muda wa kufika Kumasi, Al Ahly wanaongoza Kundi D wakiwa na alama 6, wakifuatiwa na Belouizdad akiwa na alama 5 sawa na Yanga na mwisho ni Medeama mwenye alama 4.

Post a Comment

Previous Post Next Post