🔴MAKONDA AFIKA MPAKANI KWA TANZANIA NA ZAMBIA (TUNDUMA - NAKONDE) KUJIONEA UTOAJI HUDUMA KWA MADEREVA WA MALORI.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda usiku wa saa 8 kuamkia leo tarehe 7 Februari, 2024 amefika mpakani mwa Tanzania na Zambia eneo la (Tunduma - Nakonde) kujionea namna huduma zinavyotolewa na Maafisa wa Uhamiaji kwa madereva wa malori wanaovuka kwa shughuli za usafairishaji bidhaa mbalimbali.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Mwenezi Makonda kupokea kero ya Madereva jana tarehe 6 Februari, 2024 alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika Mji wa Tunduma Mkoani Songwe.
Makonda amezungumza na Madereva katika eneo hilo ambapo walimbainishia kuwa wanapofika eneo hilo na kuonesha risiti walizolipia bado wanasumbuliwa.
"Tunafika hadi hapa vizuri, tunaonesha risiti zetu kupitia simu tizolipia passport lakini wanasema hawaoni vizuri na hata hapa Mwenezi jaribu kutazama uone na wanaposema hivyo tunawaomba hata wafanye mawasiliano

Post a Comment