Na Paul Kayanda
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga Hamis Katimba amesema kuwa kutokana na Madiwani wake kulidhishwa na utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maji inayotekelezwa na Wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira RUWASA katika halmashauri hiyo kwamba jukumu la madiwani hao ni kuhakikisha kuwa wanafanya jitihada ya kuhamasisha jamii kujua hiyo ni miradi ya Serikali na imetumia pesa nyingi ili kuzuia uharibifu wa miundombinu yake.
Katimba amesema kuwa wananchi wanapaswa kulinda miundombinu hiyo kwa sababu ni faida yao na kuongeza kuwa Serikali chini ya Raisa Dkt. Samia Suluhu Hassan imejikita kuhakikisha kuwa inamtua mama ndoo kichwani na kwamba wao wenyewe wamekuwa wakishudia miradi mingi ya maji imekuwa ikitekelezwa kwenye Halmashauri hiyo.
“Lengo la serikali imeweka miradi hiyo ili miundombinu yake itunzwe na kukaa muda murefu ili wananchi wanufaike na miradi hiyo, kwa mana hiyo ninyi Madiwani mnajukumu la kuhakikisha miundombinu ya miradi yote ya maji inatunzwa na si vinginevyo,” amesema Hamis Katimba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama.
Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Msalala Hamis Katimba, ameyasema hayo kwenye kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo huku akitoa onyo kwa wafugaji wa mifugo mbalimbali kuwa makini na mifugo yao inayotajwa kufanya uharibifu wa miundombinu ya bara bara licha ya kipindi hiki kuwa na mvua nyingi za masika ambazo nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu huo.
“Ndugu zangu wafugaji tuhakikishe tunakuwa na maeneo yetu ya kupitisha mifugo ili isiwe inapita kwenye barabara, lakini pia kwa shughuli za kilimo kuna baadhi ya wananchi wanalima kandokando ya barabara zetu naomba jamani tulinde miundombinu hii muhimu ya maji nay a barabara ili tufanikiwe kunufaika katika Nyanja za elimu, maji na uchumi pia,” amesema.
Pastory Mnyeti ni kaimu Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)katika Wilaya ya Kahama akizungumza na Sema Swahili mara baada ya kikao hicho cha baraza la Madiwani anasema kuwa hii ilikuwa ni siku ya bajeti kwa upande wa wadau kwa maana ya RUWASA na TARULA na wameweza kuwasilisha kwa ujumla mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kaimu meneja huyo anaendelea kufunguka kwa chombo hiki cha Habari kuwa lakini mapendekezo ya bajeti yalifanyika kwa kushirikisha Madiwani ambao ndiyo wanaokaa karibu zaidi na wananchi lakini ndiyo wanaojua mahitaji ya wananchi wao hatua ambayo RUWASA imepongezwa na Madiwani hao kwa utekelezaji wa miradi lukuki ya maji katika maeneo yao.
“Sisi bajeti yetu imejikita katika miradi inayoendelea, ili tuhakikishe inakamilika kwa wakati na ianze mara moja kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi lakini pia kwa miradi mipya na zaidi kuendelea kufanya utafiti wa maji chini ya ardhiili kuweza kupata vyanzo vya maji pamoja na mambo mengine,” anasema Kaimu Meneja huyo wa RUWASA.
Aidha anabainisha kuwa kikubwa kabisa wanaendelea kumshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwapatia fedha na wao kuendelea kujenga miradi bora ya maji lengo ni changamoto ya huduma ya maji safi na salama kwa wananchi iishe kabisa jambo ambalo litawezesha wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za kiuchumi katika maeneo yao.
Kuhusu bajeti ya mwaka 2024/2025 kaimu Meneja huyo anasema kuwa wamependekeza kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 10.2 ili kupunguza changamoto katika maeneo yote ya miradi iliyoainishwa na kwa miradi inayoendelea ilitengewa kiasi cha shilingi Bilioni 5.3 ambapo kufikia mwezi Disemba mwaka 2023 walipokea bilioni 2.7 na kwamba ndizo zinazoendelea kutumika mpaka sasa katika miradi ya maji.
“Niwashukuru sana RUWASA kila mmoja amezungumza vizuri na Madiwani tumeelewa kabisa, Mhe. Mwenyekiti mpaka muda huu wewe mwenyewe umeona kabisa madiwani wameridhika na kikao kimetulia, sisi madiwani tusipolidhishwa huwa tunapaza sauti kupinga kinachosemwa lakini kwa hili la RUWASA binafsi sina neon naamini na madiwani wenzangu nao wameridhika,” amesema Diwani wa Kata ya Mwakata Siksi Ibrahimu.
Pia Diwani huyo amemtaka Kaimu Meneja wa RUWASA aendelee kujituma kwa kushirikisha Madiwani wa maeneo husika, huku wakimpongeza kwa Taarifa yake aliyoiandaa na kwamba Madiwani wameikubali kwakuwa ipo kwa vitendo.



Post a Comment