Chanjo Surua,Rubela Kwa Watoto Yaanza Dodoma

  Serikali kupitia Wizara ya Afya wameridhia kufanyika kwa chanjo ya Surua rubela kwa watoto wote kuanzia miezi 9 hadi 59



Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Februari 14,2024 jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamle amesema kuwa chanjo hiyo inatarajia kuanza kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 18 Mwaka huu.

"Katika Mkoa wetu wa Dodoma idadi ya watoto watakaoenda kupata chanjo hiyo wanakadiriwa kufikia laki nne elfu ishirini na sita Mia tisa tisini na nne"Amesema

Aidha amesema kuwa vituo vitakavyoenda kutoa huduma hiyo ni vituo Mia tano arobaini na tatu,ikijumuisha vituo vya mkoba ambao pia watapita maeneno mbalimbali yenye mkusanyiko mkubwa

Kuhusu maandalizi ya utoaji wa chanjo hiyo Senyamle amesema kuwa yamekamilika ikiwa ni pamoja na kupeleka vifaa kwenye vituo husika.

Katika hatua nyingine Senyamle ametoa wito kwa wazazi,walezi na wote wenye watoto wa umri husika kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye vituo husika ili waweze kupata chanjo hiyo



Kwa upande wake Mratibu wa chanjo Mkoa wa Dodoma Fransic Bujiku amesema kuwa chanjo hiyo itatokewa katika vituo vya kutolea huduma,na maeneo maalum yaliyoandaliwa

"Tayari tushaandaa maeneo maalum hivyo watoto watapelekwa kwa ajili ya kupata huduma ya chanjo"

Aidha amesema kuwa Wakati wa utoaji wa chanjo ya kampeni hii utahusisha vituo vya kutolea huduma ya afya na huduma ya mkoba sababu kubwa ya kutumia huduma ya mkoba amesema kuwa kuna watoto wengine wanaishi sehemu za vitongoji,pia watakuwa na kliniki tembezi mahususi kwa wale watoto watakaokuwa maeneo ya mbali na vituo kwa hiyo watoa huduma watawafata maeneo yao ili waweze kupata chanjo

Ameongeza kuwa Wakati wa utoaji wa chanjo utahusisha maeneo mbalimbali ikiwemo masoko,shule, nyumba za ibada,vituo vya mabasi na maeneo mengine.

Pia amesema kuwa chanjo hii itafanyika kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 18 mwezi huu yenye kauli mbiu Surua rubbela Onesha Upendo Mpeleke mtoto akapate chanjo.


Post a Comment

Previous Post Next Post