Waziri Wa Utalii Zanzibar Ajiuzulu



Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt. Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.




“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni. Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.”  - sehemu ya taarifa yake ya kujiuzulu

Post a Comment

Previous Post Next Post