Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Suleimani Jafo amewaasa wananchi kutumia vizuri kipindi hichi cha mvua kukijanisha nchi ikiwa ni ajenda kuelekea tarehe 26 Aprili miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa zoezi la upandaji miti na wadau mbalimbali katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Aidha ameongeza kuwa hali ya mabadiliko ya tabia nchi imekuwa kubwa sana na ukienda maeneo mbalimbali hali sio shwari hivyo wananchi wanakila sababu huhakikisha wanatunza mazingira.
“Kila mtu apande miti na ikumbukwe mwaka jana mwezi wa 3 tulitoa tangazo la Serikali ambayo hayo ni maelezo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alipofanya mkutano mwezi oktoba mwaka 2022 mkutano wa nishati safi ya kupikia alielekeza taasisi za umma na taasisi binafsi zianze mchakato wa kubadili matumizi ya kuni na mkaa,ndio maana mwaka jana tulienda katika kuhakikisha kwamba tunaenda kutoa tangazo la serikali ambalo litaainisha kwamba utaratibu wa matumizi ya kuni na mkaa,itapofika Januari 30 2024 taasisi zenye watu kati ya 100 hadi 300 kuhakikisha wanahama kutumia matumizi ya kuni na mkaa”Amesisitiza Waziri Jafo.
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Khamisi Hamza Khamisi amesema kuwa ni wajibu wao kama ofisi kuelekeza fikra na mawazo ya Rais katika suala zima la uhifadhi wa mazingira,Serikali imeshaelekeza na kumekuwa na kampeni mbalimbali za utunzaji na uhifadhi wa mazingira sambamba na kuelimisha wanachi kupanda miti kwa wingi kupitia kampeni ya soma na miti ambapo lengo na madhumuni ni kuhakikisha wanafunzi wote kuanzia msingi mpaka chuo kikuu wanapanda miti ili kutunza mazingira kuyatunza na kuyahifadhi.
“Tutaendelea kuelimisha wananchi matumizi sahihi ya nishati mbadala ya kupikia ili lengo na madhumuni tuhakikishe kwamba tunatunza na kuhifadhi mazingira yetu tuache kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa na kuendelea kuhamasisha wengine lengo na madhumuni wananchi wao Andre miti hata kwenye matukio madogo madogo ya kijamii,jana tulikuwa JKT na tuliwaambia watu hebu tuige mfano mzuri wa mama Samia baada ya kusema tunakata keki kubwa sasa twendeni tukapande miti,ikitokea tumeoana Bibi na Bwana harusi tupande miti hata tukiachana twendeni tukapande miti”
MWISHO.
Post a Comment