Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (MuunganonaMazingira)
Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi ofisini kwa Waziri jijini Dodoma.
KatikamazungumzohayoMhe.
Dkt.
Jafo amempongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo ambapo amemuahidi ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.
Pia, amesema ufanisi wa Baraza hilo katika kazi ni matokeo ya ushirikiano kati ya wafanyakazi na kiongozi wao hivyo ametoa wito kudumisha ushirikiano baina yao ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Dkt.
Jafo amesema kuwa Serikali siku zote
inahamasisha uwekezaji hapa nchini kutoka kwa wawekezaji mbalimbali hivyo mkurugenzi mkuu anawajibu wa kusimamia suala hilo.
Aidha,
Waziri Dkt. Jafo pamoja na kuwapongeza na kuwatia moyo watendaji wa Baraza hilo pia amewataka kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ili waendelee kunufaika nazo.
Kwa upande wake Dkt.
Semesi ambaye aliambatana na wakurugenzi wakurugenzi na vitengo kutoka NEMC
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa imani yake kwake.
Amemuahidi Waziri Dkt.
Jafo, Ofisi ya Makamuwa Rais na Serikali kwa ujumla kuchapakazi kwa bidii ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi kuhakikisha hifadhi endelevu ya mazingira.
Itakumbukwa kuwa,MkurugenziDkt.
Semesi aliteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo akichukua nafasi ya Dkt. Samuel
Gwamaka ambaye muda wake ulikwisha.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment