Na Paul Kayanda, Mbogwe
Mkutano wa Diwani wa Kata ya Nyakafuru Wilayani Mbogwe Mkoani Geita, Paul Ngusa umeingia Dosari baada ya wananchi wake kuonyesha mashaka katika upatikanaji wa maeneo pamoja na matumizi ya fedha za Miradi ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bugegere iliyoko katika Kitongoji hicho.
Wakizungumza katika Mkutano wa Hadhara mbele ya Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga Wananchi wa Kitongoji cha Bugegele Kijiji cha Shinyanga ‘A’ walilalamikia mambo mbalimbali ikiwemo ubovu wa Miundombinu na kumtaka Mbunge kutolea ufafanuzi wa malalamiko yao
Kufuatia malalamiko hayo Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga aliwaagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU Wilaya ya Mbogwe kuhakikisha kuwa wanachunguza Tuhuma za Matumizi ya Fedha za Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bugegere.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo TAKUKURU wanapaswa kuchunguza Tuhuma za Matumizi ya Sh Mil 584 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bugegere.
Akizungumza mbele ya mgeni rasmi, Diwani wa Kata ya Nyakafuru Paul Ngusa alimtambulisha Mbunge wa Jimbo la Mbogwe kuhusu taarifa ya ujenzi wa Shule kutokana na fedha zilizotolewa nchi nzima na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Ngusa alitolea ufafanuzi wa namna Serikali ya Kijiji ilivyoamua kubadili matumizi ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi na kufanyika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bugegere ambayo itapokea wanafunzi zaidi ya 300 katika kipindi hiki cha 2024.
Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Nyakafuru Paul Ngusa aliwatangazia wananchi kufanya maandalizi ya kupokea wanafunzi wanaotarajia kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2024 katika Shule hiyo mpya iliyoko katika Kata hiyo.
“Tumeamua kuhodhi eneo hili ili kunusuru fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari nchi nzima”alisema Diwani Ngussa.
Naye Edward Ntegele mkazi wa Bugegere alimtaarifu Mbunge wa Jimbo la Mbogwe kuhusu kutotajwa kwa Zahanati ya Bugegere ukosefu wa Miundombinu ya barabara na kumtaka Mbunge kusimamia ujenzi wa barabara pamoja na kutolea ufafanuzi juu ya kukwama kwa uimarishaji wa Miundombinu ya barabara.
Akitoa taarifa ya namna upatikanaji wa maeneo Mjumbe wa Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela Mussa Mwenyekiti Mstaafu wa Kitongoji cha Bugegere Abednego alieleza wasiwasi wake kuhusu namna ya ualikaji wa Mkutano wa wananchi huku akilalamikia ununuzi wa eneo lenye Ekari 8 ambalo lilipatikana na kueleza kuhusu Ofisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe alivyoingiza michoro yake na kudai kuwa eneo hilo halifai jambo ambalo lilimshangaza.
“Niombe Diwani wetu awe wazi ni kwa nini kuna kizungumkuti hasa namna upatikanaji wa eneo hilo ambapo awali ilikuwa iwe Shule ya Msingi na badala yake ikabadilishwa kuwa Shule ya Sekondari jambo ambalo tunaomba kabla Shule hii haijakabidhiwa tuwe tumekabidhiwa eneo la Shule ya Msingi” alisema Abednego.
Diwani huyo ambaye ni mwakilishi wa wananchi amekuwa ni changamoto kwa watendaji wa serikali kwa kuingilia mamlaka ya kiutendaji ikiwemo kuwalazimisha kutimiza matakwa yake kwa maslahi binafsi jambo ambalo linapelekea Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo kulumbana vikali na kusababisha ahamishiwe kituo kingine cha kazi.
Habari za ndani zinaeleza kuwa hivi karibuni Diwani huyo alitaka kuhodhi eneo linapopita Mradi wa bomba la Mafuta ili aweze kulipwa fidia kama ambavyo aliwahi kushiriki suala la Ardhi katika kitongoji cha Nyambogo yalipokuwa yamepatikana Mawe yanayosadikiwa kuwa na Dhahabu ambapo Ofisa Mtendaji huyo wa Kata alipinga vikali jambo ambalo liliibua mgogoro mkubwa kushtakiana kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela.
Hata hivyo imeelezwa kuwa Diwani huyo amekuwa na matukio mengi yanayoashiria ubabe hasa anapopingwa mawazo yake hivyo kulazimika kutumia kila mbinu ilimradi afanikishe jambo lake hasa kunapokuwa na maslahi makubwa.
“Kuhusu kuhodhi eneo linapopita Mradi wa bomba la Mafuta ili niweze kulipwa fidia
Kwamb a dili hilo liliyeyuka baada ya Ofisa Mtendaji wa Kata kukataa,ndipo nikamhamisha,kwani mimi nimekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri?nadhani ili upate taarifa ya kuhamishwa Watumishi mtafute Mkurugenzi,je uamaanisha na huyu Ofisa Mtendaji aliyekuja badala yake tulicheza naye Dili?,” alihoji Diwani Ngussa.




Post a Comment