Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke(TRRH) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeendesha zoezi la upimaji wa afya wa bure eneo la mbagala katika viwanja vya Zakhiem leo ikiwa ni njia ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wa eneo hilo wamepata fursa ya kukutana na madaktari Bingwa wa magonjwa ya ndani, wanawake na uzazi, pamoja na upasuaji kutoka hospitali hiyo pamoja na uchangiaji damu wa hiari. Zoezi hilo pia limehusisha matibabu ya macho kutoka hospitali ya wilaya ya mbagala pamoja na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda ambae ndiye mgeni rasmi wa zoezi hilo amefurahishwa na zoezi hilo na kusema kuwa hakika hivi ndio njia sahihi ya kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Mhe. Rais. Kwani kupitia uchangiaji wa damu wa hiari uliofanyika hapa unaenda kuokoa maisha ya kina mama wengi katika jamii zetu wakati wa kujifungua.
Mhe. Mapunda ametoa pongezi kwa waganga waliopo katoka wilaya hiyo kuanzia mganga mkuu wa wilaya na waganga wafadhi walioweza kufanikisha zoezi hilo.
Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt Joseph kimaro amesema ni wajibu wetu kama watoa huduma wa afya kuhakikisha tunahudumia wananchi kwa weledi na kuwafikia kwa Karibu zaidi, hivyo ametumia siku hii maalumu ya leo kupima afya za wananchi na kutoa ushauri wa kibingwa kupitia madakatari bingwa kutoka hospitali ya temeke. Ameendelea kufafanua huduma zilizokuwa zikiendelea kutolewa ni kama vile uchunguzi wa macho, kisukari, afya ya uzazi wa wanawake,huduma za lishe, utoaji wa chanjo ya UVIKO, kupima VVU, pamoja na uchangiaji wa damu wa hiari


Post a Comment