Mwenyekiti wa Club ya Simba SC, Murtaza Mangungu amesema fedha ambazo Wapenzi wa Club hiyo walichanga kwa ajili ya ujenzi wa uwanja zimetumika kujenga ukuta wa uwanja wa Bunju na nyingine zimetumika kuimarisha kambi ya Timu.
Akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa Club hiyo leo Jijini Dar ss salaam, Mangungu amesema “Kama mnakumbuka mlichanga pesa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na pesa ile ilitumika kujenga ukuta wa uwanja wa Bunju na pesa nyingine zilitumika kuimarisha kambi ya Timu”
“Tujenge Simba imara kwa kizazi cha sasa na baadaye, tuendelee kushirikiana na naamini Mwenyezi Mungu atatutangulia”

Post a Comment