🔴_Rais Museveni ayataka mataifa tajiri yakuze uchumi wa mataifa yanayoendelea.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) katika mkutano wa 19 uliomalizika jana Januari 20, 2024, Kampala, Uganda pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuhakikisha wanaimarisha uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda ili kukuza uchumi.
Waziri Mkuu ambaye anamwakilisha Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo jana Jumamosi, Januari 20, 2024 mjini Kampala, Uganda baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali zisizofungamana na Upande wowote (NAM) ulioanza tarehe 15 - 20 Januari, 2024. Katika mkutano huo Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museven alikabidhiwa uenyekiti wa NAM.
Post a Comment