Mlipuko wa Magonjwa ya kuhara na kutapika Mgodi wa Nyakafuru watahadhalishwa.

 Na Paul Kayanda, Mbogwe


WACHIMBAJI wanaoishi katika eneo la Mgodi wa Nyakafuru chini ya kikundi cha Isanjabadugu katika Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita wameutaka uongozi wa mgodi huo kuwekeza katika kuimarisha miundombinu ya barabara pamoja na usafi wa mazingira  kwenye eneo la makazi ya watu ili kuepusha ugonjwa wa Kuhara na kutapika.



Hatua hiyo imeelezwa na Wachimbaji hao baada ya waandishi wa habari kutembelea Mgodi huo ili kujionea namna utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed baada ya kuripotiwa kuwepo kwa mlipuko wa Ugonjwa wa kuhara na kutapika katika moja ya tarafa za wilaya ya Mbogwe Mkoani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed alipotafutwa ili kuzungumzia taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa kuhara na kutapika katika Wilaya yake alikiri kuwa na taarifa na kusema mara baada ya kupata taarifa alichukua hatua za haraka na kukaa na watendaji wa Serikali na na kutoa maelekezo ya kusambaza tahadhari hiyo kwa wananchi wote ili kuzingatia kanuni za Afya na matumizi sahihi ya vyoo.



 

“Ni kweli zipo taarifa za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kuhara na kutapika, mara baada ya kupata taarifa nimeitisha kikao cha dharula na watendaji wa Serikali na nimetoa maelekezo kwa wananchi wote kuzingatia kanuni za Afya na matumizi sahihi ya vyoo”amesema DC Mohamed.



 

Akizungumza na waandishi wa habari mganga mkuu wa Wilaya ya Mbogwe dr. zakayo Sungura aliitaja tarafa ya Masumbwe kuwa ndiyo iliyoripotiwa kuwa na wagonjwa wa kuhara na kutapika ambapo mpaka sasa kimeripotiwa kifo cha mtu mmoja kati ya watu saba wenye dalili za ugonjwa huo.

“Ni kweli tumepokea kesi saba za watu walio na dalili za ugonjwa wa kuhara na kutapika zilizoripotiwa katika Kituo cha Afya Masumbwe na mmoja wa wagonjwa hao alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Masumbwe”alisema Dr Sungura.

 

Katika taarifa yake Dr Sungura alibainisha kwamba wagonjwa hawa wametokea katika maeneo ya Shinyanga “B” huku ikielezwa kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi kuwa ni Tarafa ya Masumbwe.



 

Akitoa takwimu za kuenea kwa ugonjwa huu Dr Sungura alisema hajapata kesi yoyote kutoka katika maeneo ya Tarafa zingine lakini tayari kikao cha dharula kimekaa chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed na kutoa maelekezo ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

 

Kwa mujibu wa Dr Sungura wameanzisha Kampeni ya uhamasishaji matumizi ya vyoo na kufanya msako kubaini familia ambazo hazina vyoo na wakibaini wahusika watachukuliwa hatua kali.

 

“Baada ya kutokea kwa mlipuko huu tumefanya kikao na Mkuu wa Wilaya pamoja na watendaji wa Serikali na kwamba tumepokea maelekezo ya namna tuakavyofanya kazi kama timu ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huu”alisema Dr Sungura.

Hatua zimeelekezwa.



 

Katika hatua nyingine Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Dr Zakayo Sungura aliwataka Watumishi wanaofanya kazi katika  Migodi kujisaidia kwenye vyoo kuliko kujisaidia vichakani,kuchemsha maji ya kunawa,kutunza Mazingira kwa kufanya usafi kuandaa chakula katika mazingira safi.

 

Ili kukabiliana na mlipuko huo Dr Sungura alisema baada ya kuona namna ambavyo maandalizi ya pombe za kienyeji hayaridhishi tayari wamefungia Vilabu vyote vya pombe za kienyeji na juice za miwa kutokana na maandalizi duni yanayoweza kusababisha athari kwa watumiaji.

 

Akitoa ufafanuzi huo  Dr. Sungura alisema kesi ya kwanza ya mlipuko wa ugonjwa huu,  mgonjwa wa kwanza iliripotiwa  tarehe 1.01.2024.

 

“Mpaka sasa hakukuwa na mgonjwa mpya aliyeonekana na dalili za ugonjwa huona niwaombe wananchi wote katika Wilaya ya Mbogwe kuchukua tahadhari wakati wa kuandaa chakula wachemshe maji ya kunawa na hata yale ya kuoga na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima”alisema Dr Sungura.

 

Kutokana na hali hiyo wachimbaji hao walipaza sauti zao ili mmiliki wa leseni hiyo achukue hatua za haraka katika kutekeleza agizo la mkuu wa Wilaya ili kunusuru afya za wananchi wanaoishi katika eneo la mgodi huo pamoja na wachimbaji wenyewe.

“Kwa hali kama hii ya kipindupindu,tunaomba viongozi wa Mgodi wahakikishe wanatengeneza miundombinu ya barabra, barabara kwani lipo kwenye uwezo wao, kama wanapata hela za kuendeshea shughuli za Uchimbaji leo wao wapo kikundi kikubwa tena cha matajiri wanashindwaji kuboresha miundombinu hiyo ukilinganisha na wao ndiyo wanaitumia kwa kupita na magari yao ya kifahari,” alishauri Juma Mussa.

Naye Samwel Mlyasita akizungumzia suala la Ugonjwa huo kuikumba Wilaya ya Mbogwe aalitumia nafasi ya ujio wa vyombo vya Habari kueleza kuwa Viongozi wa Mgodi wasiiachie Halmashauri pekee katika uboreshaji wa miundombinu hasa ya Mgodini kwani wanaoumia ni wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

“Pia hapa kuna idadi kubwa ya watu wa makabila mbalimbali na kutoka maeneo tofauti tofauti wanakuja kuishi katika maeneo ya uchimbaji ili kujitafutia kipato, sasa kulingana na mira na desturi wapo wengine wanapenda mambo ya usafi na wengine hawajali hata kukaa na uchafu niwaombe Mgodi wahakikishe wanatoa elimu juu ya suala la usafi wa mazingira kwa tangazo hili la ugonjwa huu tutakwisha,”wanaoishi katika mazingira ya mgodi,” aliseama Mlasita.

Hata hivyo mwenyekiti wa mgodi huo Vicenti Maige akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema kuwa uongozi wa mgod unakili kupokea maelekezo ya Mkuu wa wilaya huku akitaja kuwa mgodi huo una zaidi ya watu 800 wanaoishi katika mazingira ya mgodi huo.

“Taarifa hizi za kipindupindu sisi tulizipokea rasmi tarehe 4.01.2024, tulizipata kwa Afisa Afya wa Wilaya na Afisa mazingira wa Wilaya ya Mbogwe walituelekeza namna ya kufanya kwaajili ya kukabiliana na ugonjwa huo wa kuhara na kutapika, na sisi kama mgodi tumejipanga  kwa sababu tunatambua kipindupindu kinaua watu wengi na kwa mpigo kwa hiyo tumechukua tahadhari kama tulivyoelekezwa kwa kila yalipo makazi ya watu.



Aidha mwenyekiti huyo alifafanua kuwa watu wanaoishi katika eneo hilo ni zaidi ya 800, na idadi ya vyoo katika eneo hilo imegawanyika katika sehemu mbili kwanza ni eneo wanalofanyia kazi za uchimbaji kuna vyoo 7 lakini kwenye eneo wanakokaa wachimbaji pamoja na watu wengine wanaoingia na kutoka kuna vyoo 150 jambo na kuongeza kuwa jukumu walilo nalo ni kuhamasisha wanawe mikono pindi wanapotoka chooni ikiwemo kunywa maji ya moto na kuepuka kula vyakula vilivyopoa.

mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post