Makamu Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Chamwino na Diwani wa kata ya Buigiri Keneth Yindi akizungumza leo Januari 12,2024 ikiwa ni siku ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambapo maadhimisho hayo katika wilaya ya Chamwino yamefanyika katika shule ya msingi ya wasiona Buigiri
Makamu Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Chamwino na Diwani wa kata ya Buigiri Wilayani Chamwino mkoani Dodoma Keneth Yindi amesema kuwa uzalendo ni pamoja na kupendana wenyewe kwa wenyewe katika jamii kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali watu wenye mahitaji maalumu
Yindi amesema hayo leo Januari 12, 2024 katika shule ya msingi ya wasiona Buingiri wakati akipokea misaada ya vitu mbalimbali kutoka kwa Protocol Service Team (PST) ambao wamefika shuleni hapo kuwapatia mahitaji hayo
“Uzalendo ni kama dini mpende jirani yako kama nafsi yako unapokuwa mzalendo na haumpendi jirani yako huo sio uzalendo ,kuwa mzalendo ni kumpenda jirani yako na nchi yako”Amesema
Aidha Yindi amebainisha baadhi ya sifa za kuwa mzalendo ikiwa ni pamoja na kujenga nchi,kutimiza yale majukumu ambayo umepewa na serikali au taasisi katika kuwatumikia wananchi,hali kadhalika kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo husika ambazo zinajenga na kulinda hali ya usalama
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Protocol Service Team (PST) Wilayani Chamwino Hussein Hussein amesema kuwa uwepo wa timu hii ya PST ni kutokana na maono makubwa ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Gift Msuya na tayari timu hii imefanya matukio mbalimbali na kuaminika na wapo maafisa ambao walishiriki kutoka huduma katika zoezi la ufunguzi wa ikulu ya Chamwino
Aidha amesema baadhi ya maafisa wameweza kushiriki katika dhifa mbalimbali za Serikali na Chama vikao pamoja na mikutano inayoandaliwa na wizara mbalimbali
“Uwepo wetu hapa ni mwendelezo wa mpango wetu wa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo shule ya msingi ya Buigiri wasiona na sehemu ya kwanza ya mradi ni kuanza na shule themanini na nne 84 za mkoa wa Dodoma kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu”Amesema
Akitoa salaam za Chama Cha Mapinduzi Wilayani Chamwino katibu wa chama hicho wilayani hapo Ibrahim Mpwapwa ameeleza kuwa uzalendo unatufundisha mambo mengi sana na kuna baadhi ya watu ambao sio wazalendo katika nchi yao na kuwaomba kuendelea kuwa wazalendo katika nchi
Amesema leo tupo katika shule hii yenye watoto wenye mahitaji maalumu,niendelee kutoa wito kwa wazazi na walezi kama una mtoto ambaye anauhitaji wa mahitaji maalumu mlete katika shule hii iliaweze kupata haki yake ya elimu
Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar Wilayani Chamwino yamefanyika katika shule ya msingi ya wasiona Buigiri na yameratibiwa na Protocol Service Team (PST) na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino kwa kushirikiana Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambapo katika maadhimisho hayo PST wamegawa vifaa vya shule kwa watoto wenye mahitaji maalumu na zoezi la upandaji miti
Post a Comment