Mdau wa soka, Msemaji maarufu na wa Viwango vya juu Nchini Tanzania Haji Sunday Manara leo amefunga ndoa na Mpenzi wake Mwigizaji ZaiylissaMbagala Jijini Dar es salaam.
Manara ambaye ni Mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yao, amefunga ndoa hii ikiwa ni siku sita baada ya kumvisha pete Zai, siku sita baada ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa ( January 18) lakini pia ni siku sita toka atamke mbele ya hadhira ya Watanzania kwamba angependelea penzi lake na Mrembo huyu ndio libebe ndoa yake ya mwisho maishani.
Manara ambaye alizaliwa Amsterdam, Uholanzi miaka ya 70 mwishoni, siku sita zilizopita alitamka yafuatayo “Ndoa zote nilikua nataka ziwe za mwisho lakini binaadamu wanapita katika mitihani sasa katika hii naomba Mungu anivushe mitihani hii ndio iwe ndoa yangu ya mwisho, sio sifa nzuri kusifiwa kuoa hata kama sheria inaruhusu, kimaadili sio sifa nzuri”
Kuanzia November mwaka 2023 wawili hawa walianza kuonesha ukaribu wao kupitia mitandao kwa kuitana Kaka na Dada lakini baadae kama wasemavyo "penzi ni kikohozi kulificha huliwezi"……walikiri hadharani kwamba mahaba ni shatashata na leo hatimaye wamefunga ndoa.


Post a Comment