Dkt.Kiruswa Kutembelea Kiwanda Cha Kuchakata Madíni Ya Kinywe


🔴Kiwanda kimefanikiwa kuchakata Madini ya Kinywe tani 22,357.25 kwa miaka 2.


🔴 Kiwanda kinachenjua tani 100 za Madini ya Kinywe kwa siku.


Na.Samwel Mtuwa - Tanga


Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa leo Januari 16, 2023 ametembelea kiwanda cha kuchakata na kuzalisha madini ya kinywe kilichopo wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambapo ameshuhudia shughuli mbalimbali za uzalishaji zikiendelea.



Akizungumza katika mkutano na wafanyakazi wa kiwanda pamoja na  Uongozi ,  Dkt.Kiruswa amefafanua kuwa serikali inaandaa mpango mkakati utakaoelekeza katika mnyororo mzima wa shughuli za uchimbaji na uchakataji wa madini mkakati wenye lengo la  kuhakikisha  shughuli zote za uchakataji zinafanyikia hapa nchini. 


Naye , Mkurugenzi wa kiwanda hicho Godlisten Mwanga ambaye ni Mtanzania amesema kuwa uzalishaji rasmi wa madini ya kinywe ulianza mwaka 2021 ambapo kufikia   mwaka 2023 kiwanda kimefanikiwa kuzalisha jumla ya tani 22,357.


Mwanga ameongeza kuwa mpango wa awali ulikuwa kuzalisha tani 78,000 lakini kutokana na changamoto za nishati ya umeme na miundombinu ya barabara imeshindikana kufikia wastani  huo.



Kwa upande wake,  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando amesema  kuwa kiasi cha bilioni 50 tayari kimetengwa kwa ajili ya kusimika mitambo ya uzalishaji wa nishati ya umeme  itakayo elekezwa katika sehemu za migodi ya uzalishaji madini.

Post a Comment

Previous Post Next Post