BIL. 18 kusambaza umeme Migodini Nyang’hwale.

 

Na Paul Kayanda, Nyang’hwale


SERIKALI Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 18 kwaajili ya kusambaza huduma ya Nishati ya umeme katika Migodi mbalimbali katika Wilaya hiyo ili kuongeza uzalishaji na Serikali izidi kukusanya mapato yake.



Mgodi wa Isonda ulioko Wilayani hapa pamoja na wananchi wakijiji hicho wanakabiliwa na ukosefu wa Nishati hiyo jambo ambalo wamepaza sauti ili serikali itekeleze wajibu wake wa kusogeza Huduma hiyo muhimu.


Hayo yamesemwa na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Wilaya ya Mbogwe Eng.Lucas Kaloli ambapo amesema kuwa kiasi hicho kimetengwa kwaajili ya kupeleka Umeme katika hayo maeneo na mkandarasi yupo kazini kwa sasa.



Meneja huyo amesema kuwa kwa sasa Mkandarasi huyo ameanzia Igalula atoke hapo aende Mgodi wa Isonda, badae Ifugandi anamalizia Mgodi wa Bululu.


“Sisi Nyang’hwale tunamiradi mbalimbali ambayo tunatekeleza ikiwa ni moja ya sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na moja ya miradi ni kufikisha kwenye maeneo ya vijiji, tuna vijiji 62 mpaka sasa tumefikisha huduma ya Nishati ya Umeme kwenye Vijiji 59 bado Vijiji vitatu ambavyo vitafikiwa kabla ya mwezi wan ne,” amesema Meneja.


Meneja huyo amesema kuwa Serikali imeendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa Nishati hiyo inafika kwenye maeneo ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu , nia ya Serikali inapanua na kuongeza kasi ya Uchumi Nchini.



Amesema kuwa inafahamika wazi kuwa katika Wilaya ya Nyang’hwale shughuli kubwa ya kiuchumi ni eneo la Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu na kuongeza kuwa kwa kuanza wana maeneo manne, ambayo ni Igalula,Isonda,Ifugandi na Bululu na kwamba hayo maeneo ni maeneo ya Mkoa wa Geita ambayo yaliingizwa kwenye mradi unaolenga kwenye maeneo ya shughuli za Uchimbaji mdogo hususani Madini ya Dhahabu.


Wakizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea Mgodi huo Wachimbaji Abiud James Ndaula pamoja na  Sylvester Williamu wamesema kuwa kukosekana kwa Nishati ya Umeme kunawapa changamoto katika utekelezaji wa majukumu yao na kuiomba serikali kusikiliza kilio hicho.


“Tunataka tunaomba tuikumbushe Serikali huu Mgodi ulisha kuwa mkubwa tunaomba Serikali isikusanye tu mapato bali wakumbuke kutuletea Umeme hiyo itakuwa ni njia Nzuri ya kuendelea kukusanya mapato yake,” alisema James Mchimbaji.


“Wachimbaji hawa wanachangamoto kubwa ya kukosa tu Miundombinu ya Nishati ya Umeme iwapo Umeme utakuja kwenye Mgodi wetu kazi kubwa zitafanyika na Serikali itaendelea kukusanya mapato lakini kwa upande wa Miundombinu ya barabara huku barabara ni mbovu hazipitiki serikali ilichukulie pia kwa uzito fedha zinatokea huku,”alisema Sylvester Wiliamu.


Cosmas Gasper Luziga ni mkaguzi mkuu wa Usalama katika Mgodi wa Isonda Gold mine uliopo nje kidogo ya mji wa Kharumwa wilayani Nyahwale Mkoani Geita baada ya timu ya wanahabari kutua Mgodini hapo ameweza kutumia nafasi hiyo kuikumbusha Serikali juu ya changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo ambapo anaamini kwamba changamoto hizo zikifanyiwa kazi mapato ya wachimbaji na serikali kwa ujumla yataongezeka.


 



“Tunatumia gharama kubwa za uendeshai wa Mgodi kwa kutumia Nishati mbadala inayotokana na jenereta, mafuta tunayotumia ni mengi kama hiyo hela ingenunua luku kama umeme upo mgodini naamini tungechapa kazi nyingi na serikali pia ikakusanya zaidi mapato, kwaujio wenu Waandishi wa Habari naamini kero yetu itatatuliwa na tutapiga kazi



Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post