Na Paul Kayanda
Mbogwe
WAENDESHA Bodaboda Kata ya Mbogwe wilayani Mbogwe Mkoani Geita wametakiwa kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii waliyopo ikiwemo kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa hatua kali dhidi ya wahalifu.
Asilimia kubwa vijana ambao ni waendesha bodaboda ndiyo kundi kubwa lenye uwezo wa kusambaza elimu hiyo kwa haraka zaidi kutokana na kuwa karibu sana na jamii jambo ambalo jeshi hilo limetumia vijana hao kuwapa elimu hiyo.
Mkaguzi wa Polisi Kata ya Mbogwe Denis Rwehummbiza alisema hayo jana wakati alipokuwa akitoa Elimu kwa waendesha pikipiki maarufu bodaboda katika kijiji cha Nanda Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Nkoani Geita.
Mkaguzi huyo wa Polisi Kata ya Mbogwe aliwaeleza vijana hao juu ya madhara yanayotokana na vitendo hivyo ikiwemo kuathirika kisaikojia,majeraha na mara nyingine hupelekea vifo kwa watendewa.
"Ndugu zangu vifo vingi vinatokana na vitendo vya ukatili tafadhali msiwafanyie vitendo hivo wenza wenu,watoto na jamii kwa ujumla, pendeni familia zenu ,tunzeni famila zenu tengeni muda wa kuongea na famila zenu pia hiyo ni njia sahihi ya kuepuka ukatili wa kijinsia,"alisema Rwehumbiza.
Aidha mkaguzi huyo wa polisi alisisitiza kwa kuwataka kutoa taarifa za uharifu na waharifu wa vitendo hivo kwa jeshi la polisi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwani huo ni uharifu Kama uharifu mwingine.
Mwisho.


Post a Comment