Serikali imejipanga kuhakikisha Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar
(ZEMA)zinapata usajili Mfuko wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabia nchi (GCF).
Mhe. Maryam Azani Mwinyi aliyeuliza hatua za kusajili taasisi kwenye Mfuko wa GCF, bungeni jijini Dodoma leo Novemba 10, 2023.
Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na mawasiliano, majadiliano na mazungumzo ya kuhakikisha usajili kwa taasisi za Serikali unakamilika.
“Kwa sasa kwa sasa zaidi ya taasisi sita bado hazijafanikiwa kwa hiyo tunaendelea kufanya kazi ya kuwahamasisha wenzetu wa Mfuko iliwakubali maombi yetu kwa lengo sasa taasisi zetu ziweze kunufaika,” amesema.
Aidha, Waziri Jafo amefafanua kuwa NEMC
tayari imeshaomba na kuanza mchakato wa usajili tangu mwaka 2021 n aupande wa ZEMA
ilikuwa bado hajawasilisha maombi ya usajili kwenye Mfukowa GCF.
Hivyo, ameongeza kuwa Serikali itaendeelea kuhakikisha taasisi zote zinazoomba usajili katika Mfuko huozinafanikiwa kupata usajili ili kunufaika na faida zake.
Katika swali la nyongeza alilouliza kuhusu lini ZEMA wataanza usajili kwenye Mfuko kutoka na nauhitajiwa miradi ya mazingira,
Dkt. Jafo amesema kuwa kutoka na changamoto ya mazingira Zanzibar, SJMT
na Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zinashirikiana katika utetekelezaji wa miradi.
Ametaja baadhi ya miradi ni ujenzi wa miundombinu ya kuzuia mawimbi ya bahari kuingia nchikavu Sipwese Wilaya ya Mkoani,
Mkoa wa Kusini– Pemba, Mrad iwa Kuhimili Mabadiliko ya Tabia nchi kwa kutumia MifumoIkolojia(EBARR)
WilayayaKaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini naMradi wa Kurejesha Ardhi
iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula (LDFS)
unaotekelezwa katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini – Pemba.
“Naomba ni wahakikishie wabunge kwamba tutaendelea kushirikiana ili kuhakikisha pande zote mbili za Muungano ziweze kupata fursa hii ya miradi ya maendeleo hususan katika sekta hii ya mazingira,”
amesisitizaDkt. Jafo.
Post a Comment