Wanafunzi VyuoVya Kati Wakaribisha Na K K.K.T Dodoma


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki hafla ya Mkesha wa kuwakaribisha wanafunzi wa vyuo vikuu vya kati mnamo Novemba 17, 2023 ukiandaliwa na Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Dodoma na kufanyikia katika viwanja vya Kanisa Hilo Jijini Dodoma.


Mkesha huo ulioanzishwa mwaka 2012 ambao mwaka huu ikiwa ni awamu ya 12, una lengo la kuwasaidia vijana wanaojiunga na vyuo vikuu na vya Kati kuweza kukabiliana na changamoto za Maisha huko vyuoni na waweze kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. 



Kauli mbiu iliyobeba mkesha wa mwaka huu ni "USIKU WA MATOKEO CHANYA (Night of Impact Seasons)."

Post a Comment

Previous Post Next Post