Uongozi Wa Soko la Sabasaba Jijini Dodoma Waanza Kuekeleza Maagizo Ya Mwenyekiti Wa CCM Dodoma.

 

    DODOMA

UONGOZI wa soko la sabasaba Jijini Dodoma umeanza kutekeleza maagizo ya mwenyekiti wa CCM mkoa Dodoma kwa  kuanza kutengeneza njia zilizomo ndani ya soko hilo kwa kutumia kokoto na saraju ili kukabiliana na tatizo la tope nyakati za mvua pamoja na kuepuka magonjwa ya mlipuko kwa wateja wanaofika sokoni hapo



Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa soko hilo Nyamsuka  Nyamsuka  amesema kuwa hatua hiyo ni kutekeleza agizo la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa Dodoma Adam Kimbisa pamoja Serikali ya Jiji la Dodoma ambayo lengo lake ni kuweka miundombinu bora ndani ya soko ili wafanyabiashara waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.



Nyamsuka ameeleza kuwa ujenzi huo wa njia za ndani ya soko umeanza  kwa  kudhibiti maeneo yote ambayo yanakuwa kero nyakati za mvua kwa kuwa na tope na madimbwi ya maji ambapo wanaamini  shughuli hiyo itakapokamilika adha hiyo haitaweza kujitokeza.



Kwa upande wake mjumbe wa soko hilo Adam Abdalla kombo amesema kuwa ujenzi huo unagharamiwa na wafanyabiashara wenyewe wa soko la sabasaba ambapo kila mwenye banda amechangia shilingi elfu hamsini.



Post a Comment

Previous Post Next Post