Sido Dodoma Yatoa Mafunzo ya Uokaji Mtaalamu Atoka Uholanzi


SHIRIKA la Viwanda vidogo nchini (SIDO),mkoani Dodoma limewataka wahitimu wa Mafunzo ya uokaji bidhaa mbalimbali kwenda kutumia ujuzi walioupata kutoka kwa mtaalamu wa uokaji mikate kutoka nchini Uholanzi.



Mafunzo hayo ya wiki moja yameshirikisha wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini,ambao wamepata Mafunzo ya uokaji bidhaa mbalimbali za vyakula.



Akizungumza Wakati wa kufunga Mafunzo hayo msimamizi wa kituo hiko Stephan Ndunguru alisema wahitimu hao wanatakiwa kwenda kuwa mabalozi wazuri katika mikoa wanayotoka,lakini pia wakayatumie kwa vitendo ili kujiinua kiuchumi.


Alisema SIDO kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa wakiandaa Mafunzo mbalimbali ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi ambao utawasaidia kwenda kujiajiri wao wenyewe badala ya kusubiri ajira kutoka sehemu mbalimbali.



Kutokana na hilo amewataka vijana kushiriki Mafunzo mbalimbali pale yanapotangazwa na SIDO ili waweze kupiga hatua kiuchumi.



Naye Mtaalam wa uokaji mikate kutoka nchini Uholanzi Bert Steehouder alisema amekuja kutoa Mafunzo hayo kwa vijana hao,ili kuhakikisha washiriki wanafika Mbali kwenye uokaji wa bidhaa hizo.


Steehouder alisema ameona juhudi zinazofanywa na washiriki katika Mafunzo hayo ambapo amewataka kwenda kutumia ujuzi huo kwa vitendo ili waweze kusonga mbele.


Alifafanua zaidi ya kuwa hivi sasa soko la bidhaa Afrika liko vizuri ili mradi tu mtu afuate taratibu za kuhakikisha anasajili biashara yake ili aweze kutatua wigo wa soko lake.


Kwa upande wake mgeni rasmi kutoka Wizara ya Viwanda Festo Katera aliwapongeza SIDO kwa kuandaa Mafunzo hayo,huku akisisitiza washiriki wote kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa vijana wengine ambao hawajapata nafasi ya kushiriki Mafunzo hayo.


Alisema serikali imekuwa ikitoa sapoti katika Mafunzo mbalimbali ili kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kushiriki ikiwemo kuweza kujiajiri wao wenyewe.


Kutokana na hilo aliwataka washiriki wa Mafunzo hayo kwenda kuyatumia kwa vitendo ili waweze kusonga mbele katika bidhaa ambazo wamejifunza katika Mafunzo hayo ya wiki moja.


Naye Joan Boniface alisema wao TBA ambao wameahiriki katika utoaji Mafunzo hayo aliwataka vijana kutumia fursa za kujiendeleza zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kuwaendeleza vijana ikiwemo kuwainua kiuchumi

Post a Comment

Previous Post Next Post