Serikali Inamatarajio Makubwa Na Wakala WaMbegu Za Kilimo(ASA) –KAMATI YA BUNGE

 Na Lucas Raphael,Tabora


Serikali ina matarajio makubwa na Wakala wa Mbegu za kilimo ASA katika kuongeza Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo hapa Nchini.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Daniel Silo  Akipatiwa maelezo ya mradi wa umwangiliaji jinsi unavyofanya kazi kutoka kwa Mhandisi Lavet Chipunza wa kampuni ya Pro Agro Global Ltd .

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Daniel Silo  alitoa kauli hiyo Leo alipokuwa katika  Ziara ya kukagua Mradi wa Umwagiliaji wa Shamba la Mbegu Kilimi Nzega mkoani Tabora .

 

Alisema Kwa uwekezaji uliofanywa na ASA kupitia wizara ya kilimo Kamati hiyo inaimani na ongezeko la Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo Kwa wananchi.

 

Kamati hiyo imeipongeza Wakala wa Mbegu za kilimo Kwa kuonesha uthubutu wa nidhamu ya matumizi ya fedha za umma katika Miradi yote iliyotekelezwa.


WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Bajeti pamoja na mwenyekiti wa kamati hiyo Daniel Silo wakipata maelezo ya kijia juu ya mradi huo kutoka kwa  Mhandisi Lavet Chipunza wa kampuni ya Pro Agro Global Ltd .

 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde alisema wizara imedhamilia kukibadilisha kilimo kiwe kilimo Cha kisasa chenye tija kwa wananchi hasa Kwa kuwa na Mbegu bora.

 

Alisema shamba hilo la Kilimi limefungwa miundombinu ya Umwagiliaji katika Hekta 220 ambapo bado hekta 180 zinaendelea kufungwa.


Mhandisi Lavet Chipunza wa kampuni ya Pro Agro Global Ltd inayojenga miundombinu ya Umwagiliaji katika shamba la wakala wa mbegu kilimi nzega akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.

 

Alisema malengo ya serikali nikuongeza Uzalishaji wa Mbegu za kilimo ilizitosheleza na ikiwezekana kuuza nchi za nje.

 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge aliipongeza kamati hiyo ya Bajeti kwa kukagua miradi ya Wakala ilikuona thamani ya fedha za umma iliyotumika.

 

Alisema Wakala wa Mbegu utaendelea kuwa na nidhamu na fedha za umma ilikutekeleza Miradi inayopangwa na serikali.


 

Kwa Mawasiliano na SEMA B.A Media Mob:0713815108

Au Email: media32tv@gmail.com


 


Post a Comment

Previous Post Next Post