Kanisa Laomba Taifa Liwe Na Viongozi Wake Walio Bora.

 Na Peter Mkwavila DODOMA

KANISA la Gospel Christ Church Tanzania (GCC) limesema kuwa Taifa lolote ili liweze kuwa na mafanikio ya kimaendeleo ya kimsingi ikiwemo ya kielimu,kiafya kiuchumi kilimo na kiroho ni lazima kuwee na viongozi wake walio wa Kiroho na Serikali ambao ni bora.

Mkuu wa kanisa hilo Askofu Dkt Daud Chidawali alisema hayo  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,baada ya kutunukiwa PHD ya (Doctor of Divintity)  Elimu Imuhusiyo Mungu na Huduma katika Kanisa, aliyotunukiwa na Chuo cha International Christian University of Ministry Education - Miissouri - USA. katika kituo cha Mombasa Kenya.


Alisema kuwa bila ya viongozi hao bora hakuna maendeleo ya ya kimsingi kama vile ya kiroho,kielimu kiuchumi,kiafya kilimo na kijamii,hivyo Taifa ni lazima wapatikane wenye kujali mahitaji ya watu ambayo ni ya msingi kwa wanadamu wake.

Dk Chidawali alisema kuwa viongozi hao wanawajibu wa kutambua changamoto zinazowakabili wananchi wao juu ya maisha wanayoishi siku zote ikiwa ni haki yao ya msingi kama vile amani,ardhi,elimu,afya, malazi na chakula

Hata hivyo alisema kuwa Taifa nalo ili liweze kuendelea linahitajika watu wasomi hivyo ninawaomba  viongozi wa kidini na kiserikali kuhakikisha wanawaanda vijana kielimu, ili Nchi iweze kuwapata watakaopewa dhamana ya kuongoza katika sekta mbalimbali wenye maadili ya Kiroho na kisiasa na kijamii.

"Hivyo niwaombe viongozi wawe wa kidini au kiserikali ni wajibu wetu kuhakikisha suala la elimu tunaliweka kipaumbele kwa watoto wetu kwa ajili ya kuwaanda ili waweze kushika nafasi katika sekta mbalimbali za uongozi"alisema 

Alisema kuwa wakiandaliwa kwa kusomeshwa Taifa litaepukana na changamoto ya kuwapata viongozi wabovu wanaojijali wao wenyewe badala ya watu wote,pia wasiokuwa na maadili ya kiroho wapenda rushwa na wasiompenda Mungu kwa kuwa walio wengi watakuwa na tabia ya vitendo viovu.


    
Kiongozi huyo wa Kanisa aidha ameziomba jamii zenye uwezo wa kiuchumi kuwa na moyo wa kusaidia watu wenye changamoto za kimaisha wakiwemo wajane,yatima,walemavu,wazee na wanaoishi katika mazingira magumu.

Alisema kuwa jukumu hilo la kusaidia jamii hiyo ni ya watu wote na wao wanatakiwa kuisha kama wengine wenye kujiweza kiuchumi,hivyo hakuna sababu ya kuiachia serikali,taasisi na mashirika kusubiri mpaka watoe misaada hiyo ya kimsingi.

Post a Comment

Previous Post Next Post