Apandishwa Kizimbani Kwa Kosa La Kumuingilia Mtoto Wa Miaka 3 Kinyume Na Maumbile

 Kijana mmoja, aitwaye Baraka Athumani Katembe, (19) Mkazi wa Kijiji cha Mndumbwe wilayani Tandahimba mkoani Mtwara amepandishwa kizimbani  katika mahakama ya wilaya ya Tandahimba kwa shitaka la kumwingilia kinyume na maumbile,mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.


Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Joseph Julius, Mwendesha mashtaka ambaye pia ni Afisa wa polisi, Zuberi Mngodo ameeleza kuwa mnamo Oktoba 15, 2023 jioni, akiwa kijijini hapo Mndumbwe alijaribu kumrubuni mtoto huyo na hatimaye alifanikiwa kumlawiti.

Mshitakiwa alikana shitaka hilo la jinai namba 73 la mwaka huu wa 2023.

Aidha Mwendesha mashtaka aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shitaka hilo umekamilika na kuomba tarehe ya kesi hiyo kutajwa tena.

Hakimu Joseph aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 9, 2023 itakapotajwa tena kwa mara ya pili huku mshtakwia akirudishwa rumande kwa kushindwa kupata mdhamini

Post a Comment

Previous Post Next Post