Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayofadhili miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi inayotekelezwa katika maeneombalimbali nchini.
Waziri Jafo amesema kikao hicho na wawakilishi wa mashirika hayo sehemu ya ufuatiliaji wa maadhimio ya Mkutano Mkuu wa Saba wa Mfuko wa Mazingira wa Dunia – GEF, uliofanyika katika Mji wa Vancouver nchini Canada ambapo ambapo nchi zilizoendelea na zinazoendelea zilikubaliana kuwezesha ukusanyaji wa fedha katika shughuli za uhifadhi wa mazingira duniani.
Kwa mujibu wa Waziri Jafo amesema Tanzania bado ina mahitaji makubwa ya rasilimalifedha kutoka GEF kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, hivyo marabaada ya kumalizika kwa kwa mkutano huo Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais iliundatimu ya wataalamu kwa ajili ya kupitia vipaumbele vya miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kwa ajili ya uratibu wa maombi ya fedha za utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo.
“Tanzania ni mhanga mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi. Leo ukitazama Wilaya ya Simanjiro utaona ni kwa jinsi gani wafugaji wanavyohangaika na mifugo ya….Si hapo tu na Mpwapwa napo hali nayo si nzuri…Hivyo tunahitaji miradi mingi zaidi ya ufadhili wa fedha ili kuzinusuru jamii zetu” amesema Waziri Jafo.
Kwa upande wake Mshauri wa Rais, masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira Dkt. Richard Muyungi ameyashukuru mashirika hayo kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali ya mazingira hapa nchini na kuongeza kuwa mahitaji makubwa zaidi ya fedha bado yanahitaji ili kuleta manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Dkt. Muyungi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya kimataifa ili juhudi za pamoja ziendelee kuimarishwa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha miradi ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira inaendelea kuibuliwa katika jamii.
Post a Comment