Serikali kupitia Wizara ya Madini imetatua rasmi mgogoro wa wachimbaji wadogo wa madini uliodumu kwa mwaka mmoja katika Kitongoji cha Mafurungu ,Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Akizungumza leo Oktoba 10 , 2023 katika Mkutano na wachimbaji wadogo Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini inatambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo katika ukuaji wa uchumi wa taifa hivyo inafanya kila juhudi ili kuona wachimbaji wadogo wa madini wapo katika mazingira salama ya uchimbaji
Pia Mhe.Mavunde ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wachimbaji katika maeneo yao ya kazi ambapo katika juhudi za kuunga mkono maendeleo ya kitongoji cha Mafurungu tayari ametoa ahadi ya mifuko 200 ya Saruji na kuwa Balozi wa kujitolea kwa eneo hilo.
Naye Meneja Mgodi Mbwana Mosses akisoma taarifa ya mafanikio ya Chama cha UWAWAMA kuhusu uzalishaji wa dhahabu amesema kuwa hadi sasa chama kupitia migodi yake kimeweza kuzalisha kiasi cha gramu 11093.19 za dhahabu ambazo zina thamani ya TZS. 1,331,419,080.67 na kulipa Mrabaha wa TZS. 79,888,144.75.



Post a Comment